HARAMBEE STARLETS WAFUZU KWA KOMBE LA DUNIA
Kenya imefuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake walio na umri chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Burundi mabao 2-0 na hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa kufuzu kwa mikondo miwili
Marion Serenge alitangulia kufunga dakika ya 17 kabla ya Valerie Nekesa kuhitimisha ushindi huo katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ulinzi Sports Complex, jijini Nairobi.
Ushindi huo unawakabidhi Junior Starlets tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia la Fifa la wanawake walio na umri chini ya miaka 17 litakaloandaliwa na Jamhuri ya Dominika mwezi Oktoba na Novemba
Imetayarishwa na: Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































