#Athletics #Sports

BURIANI REBECCA

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amefariki dunia.

Alifariki katika Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi mjini Eldoret ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Kaimu Mkurugenzi wa MTRH Dkt Owen Menach alithibitisha kufariki jana usiku baada ya viungo vyake vyote kuharibika

Alisema hospitali itatoa ripoti kamili kuhusu suala hilo baadaye mchana

Cheptegei alipata asilimia 80 ya majeraha ya moto baada ya mpenzi wake anayedaiwa kumwaga mwili wake na petroli na kumchoma moto.

Michomo iliharibu viungo vyake vingi.

Mpenzi huyo Dickson Ndiema Marangach pia alipata majeraha ya moto wakati wa shambulio hilo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

BURIANI REBECCA

IPOA: WANAHABARI MKO SALAMA

BURIANI REBECCA

OLUNGA NJE AMA NDANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *