#Football #Sports

MBAPPE NJE YA KIKOSI

Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ameachwa nje ya kwa mechi zijazo za ifaransa kwenye ligi ya mataifa ya ulaya mwezi huu baada ya kocha Didier Deschamps kutaja kikosi chake hii leo.

Nyota huyo wa Real Madrid alirejea kutoka katika kipindi kifupi cha jeraha la paja, akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo ambao Real Madrid ilishangazwa 1-0 dhidi ya Lille kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hatashiriki katika mechi za Ufaransa dhidi ya Israel na Ubelgiji, ili kumruhusu kupumzika na kufanyia kazi utimamu wake.

Ufaransa itacheza na Israel Alhamisi ya Oktoba 10 katika mechi ya ugenini iliyohamishiwa Budapest kutokana na hali ya usalama Mashariki ya Kati.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MBAPPE NJE YA KIKOSI

KALENDA YA WANDA LEAGUE IMETOKEA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *