#Local News

UASIN GISHU YAPATA NAIBU GAVANA MPYA

Wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu wanatarajia kuimarika kwa utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo baada ya kupata naibu gavana mpya kufuatia kuapishwa kwa Evans Kapkea kujaza pengo lililoachwa na John Barorot.

Kapkea ambaye amekuwa akihudumu kama mwakilishi wadi ya Tembelio, aliteuliwa na gavana Jonathan Bii mwezi Agosti baada ya Baroro kujiuzulu.

Akizungumza baada ya kuapishwa kwake, Kapkea ameahidi ushirikiano na washikadau kutekeleza majukumu yake.

Wakati uo huo, wawakalishi wadi kwenye kaunti hiyo wakiongozwa na Moses Kebenei wameelezea matumaini yao katika uwezo wa Kapkea kufanya kazi ipasavyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UASIN GISHU YAPATA NAIBU GAVANA MPYA

WAKULIMA MACHAKOS WAPATA ‘MBEGU ZA MATUMAINI’

UASIN GISHU YAPATA NAIBU GAVANA MPYA

WAIGURU AAHIDI KUIMARISHA BIASHARA KIRINYAGA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *