BABU OWINO ADAI KUPOKONYWA WALINZI

Mbunge wa Embakasi East Babu owino amedai kupokonywa walinzi baada ya kushiriki katika maandamano ya hapo jana, akitaja hatua hiyo kama shambulizi la moja kwa moja kwa uhuru wa kidemokrasia na jaribio la kuwatishia viongozi wanaodhubutu kusimama na wakenya.
Kupitia mitandao ya kijamii, Owino ameshutumu uamuzi huo, huu ukiwa ni mwaka wa pili mfululizo kwake kuungana na wakenya kwenye maandamano.
Kwenye maandamano ya mwaka jana, mbunge huyo aliruka ukuta wa majengo ya bunge na kujiunga na waandamanaji.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa