PATRICK ODHIAMBO ATUA KCB

Klabu ya soka ya KCB imemteua aliyekuwa kocha mkuu wa Kakamega Homeboyz Patrick Odhiambo kuwa kocha mkuu mpya.
Odhiambo anachukua nafasi ya mshambuliaji wa zamani wa Hararambee Stars Bernard Mwalala kwa kandarasi ya mwaka mmoja, na anatarajiwa kuinoa KCB hadi Julai 16, 2025.
Odhiambo alishinda taji la KPL kama msaidizi wa Steven Pollack huko Gor Mahia 2019/2020.
Wanabenki hao waliachana na Mwalala baada ya kuamua kuchukua mapumziko ili kutafuta Leseni yake ya Caf A ya ukocha, hitaji la Shirikisho la Soka la Kenya katika kanuni mpya za makocha wakuu wote wa KPL.
Imetayarishwa na Nelson Andati