#Business

KENYA YAANDAA MAONYESHO YA MAUA

Maonyesho ya 11 ya Biashara ya Kilimo cha Maua ya Kimataifa yanayowaleta pamoja maafisa wakuu wa serikali, wakulima wa maua na wanunuzi kutoka nchi 75  yamefunguliwa rasmi jijini Nairobi, kufuatia wito wa uzalishaji endelevu kama vile udhibiti wa wadudu.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, katibu mkuu wa Idara ya Taifa ya Masuala ya Baraza la Mawaziri Idris Salim Dokota amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo ya siku tatu ni Uendelevu, inayowiana na dhamira ya serikali ya kukuza kilimo cha maua nchini.

Afisa mkuu mtendaji ambaye pia ni mratibu wa maonyesho hayo Dick van Raamsdonk amesema kuwa mashamba ya maua yanaelekea katika njia ya mifumo endelevu na kupunguza kiwango cha kaboni ambayo yatawezesha kuuzwa kimataifa.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi.

KENYA YAANDAA MAONYESHO YA MAUA

SARAFU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *