CITY STARS WAPATA SARE MPYA
Kayole City Stars FC imeongezewa sare mpya na Katibu Mkuu wa Utawala wa Kitaifa Raymond Omollo, iliyowasilishwa Jumapili kwenye uwanja wao wa mazoezi huko Komarock, Nairobi.
Ufadhili huo ni sehemu ya mpango unaolenga kukuza vipaji vya vijana, kutoa manufaa ya kiuchumi na kuzuia uvivu miongoni mwa vijana.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa Mpango wa Michezo wa Jamii wa Raymond Omollo Michael Otieno, alielezea maono mapana ya ufadhili huo.
Kocha wa Kayole City Stars Felix Ochieng alishukuru, akisema mengi zaidi yanaweza kuafikiwa na mipango kama hii.
Nahodha wa Kayole City Stars, Steven Odhiambo aliunga mkono maoni ya kocha wake.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































