GARETH SOUTHGATE APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate anasema Three Lions wanafahamu historia yao katika nusu fainali ya Euro 2024 wanapoelekea kwa mechi yao ya leo usiku dhidi ya Uholanzi huko Dortmund.
Vijana wa Southgate wanalenga kutinga fainali ya michuano mikubwa katika ardhi ya kigeni kwa mara ya kwanza na kufisha kikomo ukame wa miaka 58 bila kushinda michuano mikubwa.
Washindi watamenyana na Uhispania mjini Berlin siku ya Jumapili baada ya timu hiyo kutoka nyuma na kuwalaza Ufaransa 2-1 jana usiku.
England ilipoteza fainali ya Euro 2020, kwa mikwaju ya penalti kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Italia.
Nahodha Harry Kane alisema kufika fainali mfululizo itakuwa mafanikio ya ajabu kwani analenga kushinda taji la kwanza kuu katika maisha yake ya soka.
Imetayarishwa na Nelson Andati