WAKULIMA WA NG’OMBE WA MAZIWA KUNUFAIKA NA ONGEZEKO LA MAUZO YA NJE YA NCHI
Wakulima wa ng’ombe wa maziwa watanufaika baada ya Kenya kutangaza mpango wa kuongeza mauzo ya nje ya maziwa hadi KSh bilioni 9 ifikapo 2025, kutoka KSh bilioni 7.3 mwaka 2023.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Kenya (KDB), Genesio Mugo, amesema nchi inalenga masoko kama Mashariki ya Kati, Sudani Kusini na Somalia.
Serikali inapanga kusindika zaidi maziwa kuwa siagi, jibini, samli na mtindi, na kutumia mkataba wa AfCFTA kufikia masoko mapya kama DRC.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































