NCIC YAONYA DHIDI YA MATAMSHI YA CHUKI
Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa Ncic imetaka kusitishwa kwa matumizi ya lugha ya uchochezi na ya kuibua chuki inayotumika na wanasiasa na wakenya kwa ujumla katika vikao tofauti.
Katika ujumbe mwenyekiti wa Ncic Samuel Kobia anasema matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa kwenye mikutano ya kisiasa yanatishia umoja wa kitaifa.
Anasema iwapo hayatadhibitiwa matamshi haya yataleta migawanyiko na kurejesha nyuma taifa kimaendeleo.
Imetayarishwa na Maureen Amakhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































