TAHADHARI DHIDI YA WANYAKUZI, EACC

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imewatadharisha wakazi wa Nakuru kuhusiana na visa vya unyakuzi wa ardhi ambapo imeripotiwa kuwa zaidi ya ekari 164 za serikali zimenyakuliwa na watu binafsi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa EACC eneo la bonde la ufa Ignatius Wekesa, ardhi hiyo ilinyakuliwa miaka yah apo awali huku wahusika wakighushi stakabadhi za umiliki.
Hata hivyo, EACC imewataka wahusika wajitokeze na kusalimisha ardhi hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa