‘MUSYOKA NDIYE KIONGOZI WA UPINZANI’
Kiongozi wa chama cha DAPK Eugene Wamalwa amemtangaza kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kuwa kiongozi rasmi wa upinzani, akipuuzilia mbali hofu kwamba kutakuwa na mwanya wa uongozi wa upinzani kufutia kuondoka kwa Raila Odinga.
Licha ya kuunga mkono azma ya Odinga, Wamalwa na Musyoka wamesema hatua yao ya kukosa kuhudhuria uzinduzi wa uwaniaji wa Odinga umelenga kuashiria kuwa ndio viongozi rasmi wa upinzani.
Aidha, wamekariri kwamba mrengo wa Azimio hautasambaratika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































