#Football #Sports

WANYAMA AJIUNGA NA ATHLETIC FC

Nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Wanyama amefanya uhamisho wa Kiajabu hadi katika kilabu cha Dunfermline Athletic FC ya ligi ya daraja la pili ya Scotland.

Wanyama, 33, ameungana tena na Neil Lennon baada ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Kenya kucheza chini ya bosi mpya wa Dunfermline katika klabu ya Celtic kati ya 2011 na 2013.

Alishinda mataji mawili ya ligi na Kombe la Uskoti, na alifunga katika ushindi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona mwaka wa 2012 kabla ya kwenda Southampton.

Wanyama kwa miaka mitatu akiwa southmapton amecheza mechi 97 akiwa na Saints kabla ya kuhamia Tottenham kwa miaka minne.

Wakati Wanyama akiwa St Mary’s, Saints walimaliza nafasi ya nane, ya saba na ya sita katika Ligi ya Premia.

Wanyama, ambaye kandarasi yake na klabu ya MLS CF Montreal ilimalizika Januari, amejiunga na Pars hadi mwisho wa msimu kwa kutegemea kibali cha kimataifa.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WANYAMA AJIUNGA NA ATHLETIC FC

MAKATIBU WAKUU WATEULE KUHOJIWA APRILI

WANYAMA AJIUNGA NA ATHLETIC FC

MUSONYE AMEWATAKA MASHABIKI WA GOR NA AFC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *