BADILISHENI SHERIA ZA VYAMA VYA KISIASA, NATEMBEA

Katika juhudi za kulinda nafasi ya upinzani na kuhakikisha uwazi, bunge la kitaifa limetakiwa kufanyia marekebisho sheria inayohusu miungano ya vyama vya kisiasa baada ya uchaguzi.
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama waliogura chama cha Ford Kenya na kujiunga na DAP-K, gavana wa Trans Nzoia George Natembea, amesisitiza haja ya kuwepo kwa sheria inayozuia vyama vya upinzani kujiunga na serikali baada ya uchaguzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa