#Local News

SENETI YACHUNGUZA NJAMA KWENYE MKATABA WA MATIBABU WA BILIONI 6.3 KWA POLISI

Seneti imeanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa njama kati ya Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) na kampuni za bima binafsi kuhusiana na mkataba wa matibabu wa shilingi bilioni 6.3 na Huduma ya Polisi ya Taifa (NPS).

Uchunguzi huu unafuatia ripoti za ucheleweshaji au kukataliwa kwa fidia kwa maafisa wa polisi walioumia wakiwa kazini, kama inavyobainishwa katika mkataba kati ya NPS na Bima ya Afya ya kitaifa ya awali (NHIF).

Eliud Kinuthia, mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Polisi ya kitaifa (NPSC), ametoa ushahidi kwamba ni idadi ndogo tu ya maafisa wa polisi waliopokea fidia, huku madai mengi yakikataliwa au kucheleweshwa bila sababu ya wazi.

Kinuthia ameeleza zaidi kuwa NHIF imepuuza malalamiko ya maafisa walipowasilisha wasiwasi wao kuhusu ucheleweshaji na kukataliwa kwa madai hayo. Kulingana na Kinuthia, ni madai 937 tu yenye thamani ya shilingi milioni 709 ambayo yamelipwa hadi sasa.

Wakati huo huo, madai 240 yenye thamani ya shilingi milioni 240 yamekataliwa na kampuni za bima.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *