SAKATA YA KWARE: MAAFISA 8 GIGIRI WAFUTWA KAZI
Maafisa 8 wa polisi wa kituo cha Gigiri akiwemo OCS wa kituo hicho wamesimamishwa kazi, baada ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya Kware Collins Jumaisi na washukiwa wengine 12 raia wa Eritrea kutoroka kutoka kituo hicho.
Akithibitisha kutimuliwa huko, kaimu inspekta mkuu wa polisi Gilbert Masengeli amesema miongoni mwa maafisa hao ni kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Gigiri, afisa aliyekuwa kwenye zamu na walinzi.
Aidha, Masengeli amesema kuwa raia hao wa kigeni walikamatwa kwa kuwa nchini kinyume na sheria na wlaikuwa wakisubiri kurejeshwa makwao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































