ONGEZEKO LA MAAFISA BANDIA WA EACC
Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi EACC imelalamikia kuongezeka kwa tatizo la walaghai wanaodai kuwa sehemu ya Tume hiyo.
Akizungumza huko Diani, Kwale, Msemaji Eric Ngumbi amesema Tume ya EACC inakumbwa na changamoto ya ongezeko la walaghai ambao wanawalaghai maafisa wa umma na wafanyabiashara wasio na hatia.
Ameongeza kuwa watu hao wanajifanya kuwa maafisa wa EACC au vyombo vingine vya kutekeleza sheria vinavyotekeleza shughuli halali za uchunguzi.
Amebainisha kuwa tatizo hilo sasa limejikita katika kaunti za Kitui, Makueni na Machakos huku visa 24 vya walaghai vikiripotiwa kutoka eneo hilo katika muda wa miezi mitatu iliyopita.
Ngumbi aidha amesema kuwa katika Ukanda wa Mashariki ya Chini, walaghai wanaolaghai watu kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijifanya kuwa wanatoka Ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Chini ya EACC huko Machakos au Makao Makuu ya Nairobi.
Imetayrishwa na Janice Marete
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































