NAIROBI YAZIDI KUDHIBITI USAFI WA JIJI KWA MATATU NA WAFANYABIASHARA WADOGO

Serikali ya Kaunti ya Nairobi imetoa miongozo kwa wamiliki wa matatu kufuatia wasiwasi kuhusu shughuli zinazodaiwa kuzuia shughuli za usafi katikati ya jiji.
Geoffrey Mosiria, Afisa Mkuu wa Mazingira wa Kaunti, katika taarifa ameeleza kwamba maeneo mengi ya matatu yanabaki yakikaliwa na magari usiku, yakizuia shughuli za usafi.
Kama matokeo, alielekeza kwamba magari yote yaondoke katika maeneo hayo wakati wa masaa ya usafi usiku huku akiwataka wamiliki wa matatu kutunza usafi wa magari yao na kujiandikisha kwa huduma ya taka yenye leseni.
Mosiria ameonya kwamba wale watakaokiuka miongozo hiyo watachukuliwa hatua za kisheria kama inavyotolewa na sheria.
Wakati huohuo, Afisa Mkuu huyo ameonya wafanyabiashara wadogo wanaoacha bidhaa zao na mali katika mitaa na barabara ndogo kukoma la sivyo watakabiliwa kwa mujibu wa sheria
Maelekezo haya mapya yanajiri wiki moja baada ya serikali ya kaunti ya Nairobi kuwaweka wafanyabiashara wadogo kwenye barabara za nyuma za jiji.
Hata hivyo, wafanyabiashara wadogo wamejipanga kupinga agizo hilo.
Imetayarishwa na Janice Marete