SERIKALI KUSAJILI MAWAKALA WAPYA WA KUUZA KAHAWA NJE YA NCHI

Ni afueni kwa wanachama wa vyama vya ushirika vwa kahawa baada serikali ya kenya kuahidi kutoa leseni kwa vyama hivyo vya wakulima kama mawakala wa kuuza kahawa nje ya nchi, mpango ambao unaweza kuibua vita vipya vya kibiashara na wauzaji wa ndani na wa kimataifa.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kilimo na Chakula (AFA) Cornelly Serem amesema kama sehemu ya mageuzi katika sekta ndogo ya kahawa, jamii zitauza moja kwa moja mazao yao kimataifa.
Kampuni za kimataifa za kahawa zilizo na kampuni tanzu zilizoanzishwa nchini zinasafirisha kahawa nyingi nchini Kenya.
Kwa miaka miwili iliyopita, serikali chini ya ajenda ya mageuzi ya kahawa imekuwa ikipanga upya usagaji na uuzaji wa kahawa ya Kenya kama sehemu ya kuwawezesha wakulima wa ndani.
Katika maendeleo ya tasnia ya kahawa nchini, Serem amesema kuwa baadhi ya vyama vya ushirika vya wakulima vimeweza kuunganisha biashara zao kama sehemu ya kupunguza gharama na hivyo kukuza kipato cha wakulima.
Imetayarishwa na Janice Marete