TUPO TAYARI KWA MSIMU UJAO

3K FC wameongeza maandalizi yao ya kabla ya msimu mpya kabla ya mechi yao ya kwanza katika ligi ya daraja la pili nchini Kenya, National Super League (NSL).
Timu hiyo yenye maskani yake Embu ambayo ilipandishwa daraja kutoka Daraja la Kwanza, itakabiliana na mchuano wao mkubwa zaidi katika historia yao changa, lakini kocha mkuu Francis Chege anasema vijana wake wako tayari kuonyesha kiwango chao katika NSL.
Chege, ambaye alijiunga na timu hiyo ilipokuwa ikishika nafasi ya 14 katika Ligi Daraja la Kwanza na kung’ang’ania kushuka daraja, anasema bidii, na uthubutu wa timu hiyo uliwasaidia kupanda kileleni na kupanda daraja.
Chege atachuana na baadhi ya timu bora nchini na anasema hajashtushwa na kazi iliyo mbele yake, ingawa anakiri timu hiyo inahitaji wafadhili wa kuisaidia kunusurika msimu mzima wa ligi ya daraja la pili.
Timu hiyo pia inatarajia kukiimarisha kikosi chao kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa mwezi ujao.
Imetayarishwa na Nelson Andati