UTATA WA MUHURI WATATULIWA
Mwanasheria mkuu wa serikali Dorcas Oduor amesisitiza kuwa muhuri wa serikali ungali unahifadhiwa katika afisi yake ilivyo kisheria, akizima madai kwamba muhuri huo ulihamishiwa kwenye afisi ya mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei.
Kwa mujibu wa Oduor, madai hayo yanalenga kuleta mgawanyiko serikalini.
Ameyasema haya alipofika mbele ya kamati ya kurahisisha kesi za ardhi ya serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































