#Football #Sports

NGORONGORO BOYS WAICHARAZA RISING STARS 2-1

Kilimanjaro Stars ya Tanzania ndio mabingwa wa kombe la CECAFA kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 baada ya kulipiza kisasi na kuishinda Rising Stars ya kenya mabao 2-1 kwenye fainali ya Jumapili jijini Dares Salaam.

Kenya ilikuwa ya kwanza kufumania lango kunako dakika ya 48,baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare tasa ,kabla ya Valentino Kusengama kukomboa kwa wenyeji Kilimanjaro  dakika ya 65.

Sekhani Khamis alipachika wavuni bao la ushindi kwa Kilimanjaro katika dakika ya 82, huku wakilipiza kisasi cha kushindwa na Kenya magoli yayo hayo 2-1, katika mchuano wa kufungua mashindano kundini A.

Uganda Hippos walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuwacharaza Burundi mabao 3-1 mapema leo.

Tanzania na Kenya zimefuzu kuwakilisha ukanda wa CECAFA katika fainali za kombe la AFCON kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mwaka ujao.

Imetayarishwa na Janice Marete

NGORONGORO BOYS WAICHARAZA RISING STARS 2-1

SIASA ZA TAWE ZATAMBA ENEO LA MAGHARIBI

NGORONGORO BOYS WAICHARAZA RISING STARS 2-1

MAN CITY YAILAZA WOLVES 2-1 DAKIKA ZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *