MATIANG’I AHIMIZA MAZUNGUMZO

Waziri wa zamani Dr. Fred Matiang’i, amehimiza mazungumzo ya kitaifa kufanywa katika juhudi za kudhibiti machungu ya vijana na kurejesha mshikamano wa taifa.
Kulingana naye, serikali imefeli kuwasikiliza vijana, hatua anayosema huenda ikaligawanya taifa.
Naye kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, ameishutumu serikali kutokana na jinsi ilivyowashughulikia waandamanaji Jumatano iliyopita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa