EDU AHAMA ARSENALI
Mikel Arteta atapoteza mshirika wake mkuu katika klabu ya Arsenal huku mkurugenzi wa michezo mwenye sifa ya juu Edu akitarajiwa kuihama klabu hiyo.
Mbrazil huyo, kiungo wa zamani wa Arsenal, amekuwa na jukumu la kuwanasa wachezaji muhimu kama Martin Odegaard na Declan Rice na kuongoza utendaji mzuri wa Arsenal katika kusajili na kupeleka wachezaji muhimu klabuni.
Anafikiriwa sana kama mmoja wa wakurugenzi wakuu wa michezo katika kandanda ya dunia kwa kusimamia mabadiliko katika usajili wa Arsenal na pia kusaidia uondoaji wa nyota matata kama vile Pierre Emerick Aubameyang, ambao walionekana kuwa sehemu ya maisha yaliyoshindwa.
Mazungumzo yamekuwa yakiendelea na uongozi wa klabu na huku sababu zikiwa hazieleweki, ni uamuzi wake kuondoka. Taarifa zaidi zinatarajiwa kujitokeza katika muda wa saa 24 zijazo.
Edu, 46, amesema katika mahojiano kwamba anajivunia kumuunga mkono Arteta katika ‘kubadilisha jinsi watu wanavyoiona klabu na maono ya watu kuhusu Arsenal ikilinganishwa na siku za nyuma.’
Kiungo huyo wa kati wa Brazil aliyebobea, alisajiliwa na Arsene Wenger na kuchezea Invincibles na wachezaji wenzake kama Dennis Bergkamp, Patrick Vieira na Martin Keown.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































