WEZI WA KUTUMIA NGUVU WATATU WAKAMATWA ATHI RIVER
Maafisa wa upelelezi eneo la Athi River wamewatia mbaroni washukiwa watatu wanaohusishwa na visa kadhaa vya wizi na wanatarajiwa kufikishwa mahakami huku polisi wakiendelea na juhudi za kuwatafuta washirika waliotoroka, huku mali zilizopatikana zikihifadhiwa kama ushahidi
Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), waliokamatwa ni Kelvin Baraza Andayi almaarufu Kevoo, Titus Mutuku Maingi almaarufu Tush, na Jack Wilshere Kimathi almaarufu Jack, baada ya operesheni iliyoratibiwa kwa ufanisi na polisi.
Maafisa wa upelelezi wamefuatilia ushahidi wa kitaalamu na kufika katika nyumba ya kukodi eneo la Kamulu, ambapo kiongozi wa genge hilo, Kelvin Baraza Andayi, alikamatwa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































