VITAMBULISHO: VIONGOZI WAPINGA AGIZO LA RUTO

Viongozi mbali mbali akiwemo gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, wameendelea kupinga agizo la rais William Ruto la kutaka vikwazo viondolewe katika mchakato wa kutoa vitambulisho vya kitaifa kwa watu wanaotoka maeneo ya mipakani hasa Kaskazini mashariki, wakisema uamuzi huo utahujumu usalama wa taifa.
Viongozi wengine ambao wamepinga agizo hilo ni maseneta wakiongozwa na mwenzao wa Busia Okiya Omtatah.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa