#Football #Sports

BANDARI WASHABIKIA WACHEZAJI IBUKA

Kocha Mkuu Wa Bandari FC John Baraza Amewaunga Mkono Wachezaji Wake Wawili Chipukizi Izzadin Ramadha Na Willy Gitama Kufanya  vyema Msimu Ujao Baada Ya Wawili Hao Kuonyesha Mwanga Wa Kipekee Katika Mechi Za Hivi Majuzi Za Ligi Kuu Ya FKF.

Wawili Hao Walikuwa Miongoni Mwa Wachezaji Watatu Waliopandishwa Daraja Hadi Timu Ya Wakubwa Kutoka Safu Ya Vijana Mnamo Januari Kwa Mkondo Wa Pili Wa Ligi Kuu Ya FKF. Wengine  ni David Wanyama, Renson Wakalo Na Hamisi Nyale.

Izzadin, 18, Alitoka Kwenye Benchi Na Kufunga Bao La Kusawazisha Wakati Wa Sare Ya 2-2 Dhidi Ya Sofapaka Kwenye Ukunda Showground Katika Kaunti Ya Kwale Wikendi Iliyopita Huku Gitama, 17, Akitesa Timu Pinzani Katika Mechi Za Hivi Majuzi Za Ligi.

Gitama, Mwanafunzi Wa Kidato Cha Nne Katika Shule Ya Sekondari Ya Serani, Alikuwa Sehemu Ya Timu Ya Vijana Chini Ya Umri Wa Miaka 19 Ya Talanta Hela Iliyopiga Kambi Nchini Uhispania Kwa Ajili Ya Mashindano Ya Maonyesho Mwezi Uliopita, Na Alichukua Jukumu Muhimu Kusaidia Timu Hiyo Kushinda Kombe La Costa Daurada, Akiibuka Kidedea Kwenye Mashindano Yake. Meneja Wa Timu Ya Vijana Ya Bandari Abdallah Alisema Wawili Hao Wamekuwa Na Ushawishi Kwa Upande Wa Vijana, Na Kuisaidia Timu Hiyo Kutwaa Taji La Chapa Dimba Pwani. Ndiye Mfungaji Bora Wa Michuano Hiyo Akiwa Na Mabao Matatu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

BANDARI WASHABIKIA WACHEZAJI IBUKA

TIMU YA RAGA YAPATA MFADHILI

BANDARI WASHABIKIA WACHEZAJI IBUKA

REKODI YA TIGIST YAIDHINISHWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *