JULIUS YEGO AZIDI KUFANYA VYEMA

Bingwa wa zamani wa dunia Julius Yego alirusha mkuki umbali wa mita 85.97, urushaji wake bora zaidi msimu huu, na kufuzu kwa fainali ya wanaume kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 mapema leo.
Mshindi huyo wa medali ya fedha 2016 alipita alama ya kufuzu ya mita 84.0, katika jaribio la tatu la kufuzu moja kwa moja.
Bingwa huyo wa dunia wa 2015 amekuwa na panda shuka nyingi lakini aejitahidi kufikia mita 85 katika mwaka mmoja uliopita, na kufuzu kwa Olimpiki kupitia viwango vya Riadha vya Dunia.
Katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo, Yego alitolewa katika raundi ya kwanza.
Imetayarishwa na Nelson Andati