#Football #Sports

GOR MAHIA WAKO TAYARI KWA MCHUANO WAO

Kocha msaidizi wa Gor Mahia Zedekiah ‘Zico’ Otieno anasema timu hiyo haina shinikizo kabla ya mechi yao ya ligi dhidi ya viongozi ambao hawajashindwa KCB inayopangwa Jumatano.

Kocha huyo wa zamani wa KCB anasema wamedhamiria kuvunja rekodi ya timu yake ya zamani ya kutoshindwa hata kama wanalenga kupata ushindi wao wa tatu msimu huu.

Zico amepuuzilia mbali dhana kwamba wachezaji wa KCB wanamfahamu na mbinu zake alizokuwa kocha wao mkuu kabla.

Gor Mahia watacheza mechi yao ya tatu ya ligi Jumatano dhidi ya wanabenki kwenye Uwanja wa Dandora, baada ya kushinda mechi mbili za kwanza kwa jumla ya mabao 7-0. Kwa upande mwingine, KCB wamecheza mechi tano, wakishinda mechi nne na kutoka sare moja na kuwafanya wasonge mbele kileleni mwa logi kwa pointi 13.

Uma alikuwa ameomba kuondoka Gor Mahia kwa kukosa muda wa kucheza na hata kuruka vipindi vya mazoezi si kukaa vizuri na benchi la ufundi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GOR MAHIA WAKO TAYARI KWA MCHUANO WAO

MACHARIA AINGIA KATIKA MABANO YA MEDALI

GOR MAHIA WAKO TAYARI KWA MCHUANO WAO

GORDON ASEMA SHARTI ASHINDE KOMBE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *