SAFARI YA ‘CANAAN’ KWA RAILA YAANZA
Safari ya kiongozi wa Azimio kutwaa uongozi wa bara la Afrika imeanza rasmi katika ikulu ya Nairobi baada ya Rais William Ruto kumwidhinisha rasmi kuwania wadhifa wa uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC
Wakati wa hafla hiyo, Ruto ameonyesha imani yake katika uwezo wa Odinga kuongoza bara la Afrika hasa kutokana na tajriba yake katika ulingo wa uongozi.
Aidha, rais amesema kuwa Odinga atatimiza azimio ya bara hili kuimarika kiuchumi.
Wakati uo huo, Rais Ruto amezindua kamati itayoongoza kampeni za Odinga, zikiongozwa na katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































