LSK: TUNA USHAHIDI WA USHIRIKIANO WA POLISI-MAGENGE

Chama cha mawakili nchini LSK kimesema kuwa kina ushahidi wa kutosha unaonyesha kuwa maafisa wa polisi walishirikiana na magenge ya wahuni kuwahangaisha waandamanaji jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kulalamikia kifo cha bloga Albert Ojwang’.
Kwenye kikao na wanahabari, Rais wa LSK Faith Odhiambo, amesema ushirikiano huo wa polisi na magenge ya wahalifu unaibua hofu nchini.
Wakati uo huo, idara ya mahakama kupitia kwa msemaji wake Paul Ndemo, imekosoa matukio hayo yaliyosababisha kujeruhiwa kwa watu kadhaa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa