WANARIADHA WANAZIDI KUMUOMBELEZA REBBECCA
Wanariadha wamemuomboleza mwendazake Rebecca Cheptegei kama mwanariadha mwenye kipawa ambaye alitazamiwa kuwa mmoja wa wanariadha bora wa mbio za masafa marefu katika ukanda huu.
Wakiongozwa na mshirika mwenza mazoezini James Kirwa, walisema marehemu aliyefariki akiwa na umri wa miaka 33 alikuwa mkarimu na amewasaidia wakimbiaji wengine kifedha.
Cheptegei, ambaye alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya hivi majuzi ya Paris akimaliza katika nafasi ya 44, alifariki baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mchumba wake Dickson Ndiema huko Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia Jumapili iliyopita.
Babake, Joseph Cheptegei, alisema kwamba alikuwa amepoteza binti “aliyemsaidia sana”.
Cheptegei, kutoka eneo lililo nje ya mpaka nchini Uganda, anasemekana kununua kiwanja huko Trans Nzoia na kujenga nyumba kuwa karibu na vituo vya mafunzo ya riadha nchini Kenya.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































