100 WAENDA “MTEJA” KWENYE MADARAKA

Zaidi ya wakenya 100 walipoteza simu zao kwenye uwanja wa Raila Odinga mjini Homa Bay wakati wa maadhimisho ya sherehe Madaraka za mwaka huu, nyingi ya simu zikiibwa usiku umati mkubwa ulipokuwa ukiingia uwanjani humo.
Haya ni kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa kaunti ya Homa Bay Lawrence Koilem, akisema idara ya upelelezi DCI imewakamata washukiwa 2 huku simu 12 zikifanikiwa kurejeshwa.
Amewataka waathiriwa wa wizi huo kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa