#Sports

PSG WAMZIMA MESSI, INTER MIAMI

Klabu ya PSG ya Ufaransa imeibandua Inter Miami ya Lionel Messi kutoka mashindano ya FIFA Club World Cup yanayoendelea nchini Marekani, kwa kipigo cha mabao 4 bila jibu na kufuzu katika awamu ya robo fainali.

Miami waliweka matumaini kwa nyota huyo wa Argentina kuwapa ushindi dhidi ya mwajiri wake wa zamani, ila mabingwa wa bara Ulaya wakawa na nguvu zaidi na kuhakikisha kuwa msururu wao wa matokeo bora ya Ulaya unaendelezwa ulimwenguni.

Messi na wachezaji wenza wa zamani wa klabu ya Barcelona ambao ni Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba walionyesha mchezo mzuri na kuiwezesha Inter Miami wanaingia awamu ya mwondoano, ila mabao 3 ndani ya dakika 10 ya PSG yalihakikisha awamu hiyo inakuwa hatua ya mwisho wa miamba hao wa Marekani.

Joao Neves aliifungia PSG mabao 2, huku mengine yakifungwa na Tomas Avile na Achraf Hakimi

PSG sasa watakutana na vijana wa Vincent Kompany- Bayern Munich, waliowacharaza Flamengo mabao 4:2 katika mechi nyingine yah apo jana.

Mshambulizi wa Uingereza Harry Kane alifunga mara mbili, Leon Gorezka akifunga bao jingine huku kiungo wa Flamengo Erick Pulgar akijifunga bao katika dakika za ufunguzi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

PSG WAMZIMA MESSI, INTER MIAMI

NAIROBI UNITED WAINGIA AFRIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *