IEBC: RUTO APUUZA MAHAKAMA
Mwenyekiti mteule wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon na makamishna 6 wa tume hiyo wanatarajiwa kuapishwa muda wowote ili kuanza rasmi majukumu yao baada ya Rais William Ruto kuwateua rasmi kuongoza tume hiyo.
Kwenye gazeti rasmi la serikali, Rais Ruto amewateua Anne Nderitu, Moses Mukhwana, Mary Sorobit, Hassan Noor, Francis Odhiambo na Fahima Abdallah.
Hata hivyo, uteuzi huo umefanywa licha ya agizo la mahakama kumzuia Rais Ruto kufanya hivyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































