WIZARA YA USALAMA YAOMBA FEDHA

Katibu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo amesema kwamba serikali inahitaji kima cha shilingi bilioni 108 kutekeleza mageuzi katika idara ya polisi, ile ya magereza na idara ya huduma za vijana NYS ilivyopendekezwa na na jopokazi lililobuniwa na Raus William Ruto.
Kwa mujibu wa Omollo, mageuzi hayo yatatekelezwa kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu kulingana na mkakatikazi unaoongoza mchakato huo.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Omollo amesema mkakatikazi huo umebuniwa kwa mashauriano na washikadau, na itaangazia nguzo 4 ambazo ni uongozi, uwazi, uangalizi na uimarishaji wa idara hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa