MAHAKAMA KUTOA MWELEKEO KUHUSU WADHIFA WA NAIBU RAIS

Mgogoro wa uongozi katika afisi ya naibu rais humu nchini unatarajiwa kupata mwelekeo alasiri hii wakati ambapo mahakama imeratibiwa kusikiliza kesi inayotaka kuondolewa kwa amri za kumzuia naibu rais mteule Kithure Kindiki kuanza majukumu yake.
Katika kikao cha asubuhi, wakili wa seneti Tom Ojienda amewataka majaji kuipa kipaumbele kesi hiyo hasa ikizingatiwa kwamba agizo hilo la muda kutoka mahakama ya Kerugoya linatarajiwa kukamilika.
Hata hivyo, jopo la majaji 3 likiongozwa na jaji Eric Ogolla limewataka kusubiri hadi alasiri.
Aidha, jopo hilo limesema kesi zote zinazohusiana na kuondolewa mamlakani kwa naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua zitasikilizwa pamoja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa