TAHADHARI YATOLEWA KUHUSU MPOX
Unashauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Mpox ambao unazidi kuenea nchini Kenya ikiwa na zaidi ya visa 200 vya maambukizi.
Kaunti ya Mombasa imeripotiwa visa 98 hasa katika maeneo ya Nyali na Changamwe watu 2 wakiripotiwa kufariki kutokana na Mpox.
Maafisa wa afya huko Mombasa wanasema ugonjwa huo unazidi kuenea katika jamii na kuwataka wakaazi kudumisha usafi.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































