MARY MUTHONI; HAKUNA HMPV KENYA

Wakenya wamehakikishiwa kuwa wizara ya afya inafanya kila iwezalo kuthibiti maambukizi ya ugonjwa wa m-pox.
Wizara ya afya aidha imesema kuwa imeimarisha uchunguzi wa HMPV na mpox katika mipaka yote ya kenya.
Kwa mujib u wa katibu wa afya ya umma Mary Muthoni serikali imeimarisha uchunguzi wa watu wote wanaokuja humu nchini na kwamba kenya haijarekodi kisa chochote cha HMPV.
Imetayarishwa na Janice Marete