MOFA YAACHANA NA KOCHA LLYOD

MOFA FC imetangaza kuachana na kocha mkuu Lloyd Wahome baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa muda mfupi. Klabu hiyo ilithibitisha habari hizo katika taarifa ya Jumanne, ikimshukuru mtaalamu huyo kwa utumishi wake. Wahome, ambaye hapo awali aliwahi kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Murang’a Seal FC, alirejea kwa mara yake ya pili MOFA mwezi Aprili na kuchukua nafasi ya ukocha mkuu kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu, Wahome alikuwa kocha wa tatu kukiongoza kikosi cha NSL msimu huu baada ya Alfred Chole ambaye alianza msimu huu kujiuzulu kama kocha mkuu wa timu hiyo.
Mkurugenzi Kevin Aol wa kuingiliwa katika masuala ya kiufundi, jambo ambalo lilifanya msimamo wake kutokubalika.
Baada ya Chole kujiuzulu, MOFA ilimteua Charles Odera kuwa kocha wao mkuu. Odera, ambaye alijiunga kutoka Nzoia Sugar, aliongoza kwa mechi nne pekee, akishinda mbili, sare moja, na kupoteza mchezo wake wa mwisho 2-0 na Fortune Sacco.
Timu hiyo yenye maskani yake Homa Bay ilihangaika kuchukua nafasi ya Kassim Otieno ambaye walimtimua mwishoni mwa msimu wa 2023/2024 baada ya kupoteza 3-0 katika mechi ya mchujo ya kufuzu kwa NSL dhidi ya Fortune Sacco.
Kocha msaidizi wa Harambee Starlets Bruno Charles Warinda amepigiwa upatu kuchukua jukumu hilo baada ya kuondoka Kisumu All Stars baada ya misimu miwili.
Imetayarishwa na Nelson Andati