MAAFA YA MAANDAMANO

Watu 8 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine zaidi ya 400 wakijeruhiwa hapo jana kwenye makabiliano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakiadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa zaidi ya wakenya 60 wakati wa maandamano ya mwaka jana.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu Dakta Raymond Nyeris, maafa hayo yaliripotiwa kwenye kaunti 6, watu 2 wakifariki katika ya Machakos saw ana Makueni, huku kaunti za Nakuru, Kiambu, Uasin Gishu na Nyandarua zikirekodi kisa kimoja mtawalia.
Aidha, tume hiyo imefichua kupokea taarifa za maandamano hayo kuingiliwa na makundi ya wahalifu.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa