#Football #Sports

STARLETS WAFANYA MAZOEZI YA KWANZA

Timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets wamepata fursa yakufanya mazoezi yao ya kwanza kwenye uwanjani rasmi wa kuandaliwa kombe la dunia kabla ya kampeni yao ya kihistoria katika Jamhuri ya Dominika.

Starlets watamenyana na Uingereza saa nane usiku wa kuamkia Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Estadio Cibao katika mechi yao ya kwanza ya Kundi C.

Kenya itacheza na Korea Kaskazini katika mechi yao ya pili Jumapili saa tano asubuhi na kisha kumalizia mechi za Kundi C dhidi ya Mexico mnamo Oktoba 24.

Wasichana hao wamekuwa wakiimarisha mazoezi yao katika taifa mwenyeji tangu kutua salama mnamo Oktoba 2.

Imetayarishwa na Nelson Andati

STARLETS WAFANYA MAZOEZI YA KWANZA

MAJERAHA YALITULETEA HASARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *