GACHAGUA, NATEMBEYA WALILIA SERIKALI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, wamedai kwamba maisha yao yamo hatarini, wakisema serikali inawaandamana kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakiikosoa.
Katika taarifa tofauti, Gachagua amemwandikia waraka Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja akiorodhesha matukio 6 anayosema yanatishia usalama wake, ikiwemo madai ya kuandamwa na idara ya ujasusi, na njama ya kuvamia makazi yake yaliyoko Wamunyoro na Nairobi.
Naye Natembeya, amesema hana imani na idara ya usalama anayosema ina miegemeo ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa