EACC YAPATA MKUU MPYA

Wakenya wanatarajia huduma zilizoimarika kutoka kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC baada ya Abdi Ahmed Mohamoud kuapishwa rasmi kuwa afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo kuhudumu kwa miaka 6 na kujaza nafasi ya Twalib Mbaraka aliyestaafu.
Mohamoud ameapishwa na jaji mkuu Martha Koome, akiahidi kuimarisha utendakazi wa tume hiyo na kupambana na walaji rushwa.
Aidha, amehimiza ushirikiano baina ya EACC na mahakama ili kukabili ufisadi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa