CHERUIYOT AKUBALIANA NA MAGEUZI SERIKALINI

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot, amewasilisha bungeni humo hoja ambayo inaunga mjadala ulioanzishwa kufuatia maandamano ya Gen Z ya kufanyika kwa mageuzi katika uongozi serikalini.
Akizungumza katika bunge la seneti, Cheruiyot amekiri kuwepo kwa changamoto za ufisadi na maadili katika uongozi ambao umesababisha utendakazi duni na ubadhirifu wa fedha za umma.
Aidha, Cheruiyot amesema viongozi hawana budi ila kukubali kukatwa mishahara.
Kadhalika, Cheruiyot ambaye pia ni seneta wa Kericho, amehimiza kufanyiwa tathmini deni la kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa