25 WAKAMATWA, BUNDUKI 5 ZAIBWA
Polisi wametangaza kuwa wamewakamata watu 25 wanaohusishwa na uharibifu wa mali ya serikali ikiwemo afisi na mahakama ya Kikuyu kaunti ya Kiambu wakati wa maandamano yaliyoshuhudiwa siku ya Jumatano.
Kulingana na polisi, maandamano ya amani yaligeuka kuwa vurugu baada ya makundi ya wahuni waliokodishwa kutoka Limuru na Kiambu kuziba barabara ya Southern Bypass na Old Kikuyu, waliofanikiwa kuiba bunduki 5 wakati wa makabiliano na polisi.
Haya yanajiri huku jaji mkuu Martha Koome akiomba bajeti ya kuhamisha mahakama ya Kikuyu ambayo ilichomwa moto.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































