MALUMBANO YA MCAS YATATIZA SHUGHULI KWENYE KAUNTI

Wawakilishi wadi katika baadhi ya mabunge ya kaunti nchini wameendelea kutatiza utoaji huduma kwa wakazi katika kaunti hizo kutokana na hali ya kutoelewana miongoni mwao, kaunti ya hivi punde ikiwa ni ya Kirinyaga ambapo wawakilishi wadi wamezozana kuhusu uongozi wa bunge hilo na kusambaratisha shughuli za kawaida.
Hii ni baada yao kumtimua kiongozi wa walio wengi Muriithi Kibinga na kujaza nafasi yake na Geoffrey Gakuru, wakidai kwamba Kibinga ameshindwa kutekeleza majukumu yake.
Haya yanajiri wakati ambapo shughuli katika bunge la kaunti ya Nandi zimesitishwa kufuatia mzozo bungeni humo wiki jana wakati wa uwasilishaji wa ripoti kuhusu ufisadi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa