UJENZI WA AFUENI WEBUYE

Huduma za matibabu katika kaunti ya Bungoma zinatarajiwa kuimarika kutokana na ujenzi unaoendelea wa jumba la ghorofa mbili katika hospitali ya rufaa ya kaunti ndogo ya Webuye itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa unaoshuhudiwa kwa sasa eneo hilo.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka amekiri kuwepo kwa changamoto za msongamano wa wagonjwa, akidokeza kuwa kuna mikakati ya kupandisha cheo hospitali hiyo na ile ya Bungoma.
Kwa upande wake msimimizi wa hospitali hiyo David Wanikina, amekariri afueni itakayoletwa na mradi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa