MILIPUKO YA MAGONJWA KUATHIRI SEKTA ZA BIASHARA BARANI AFRIKA
Ripoti kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD) inaonyesha kuwa pembe za Afrika imerekodi ongezeko la milipuko ya magonjwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha mafuriko makubwa.
Hata hivyo, IGAD imezitaka nchi ambazo zinashuhudia milipuko hiyo kuweka mikakati kabambe ya misaada na njia za kupata fedha ili kulinda Maisha ya wananchi na kuendeleza mifumo ya Uchumi.
Kulingana na ripoti hiyo, magonjwa ambayo yamerekodiwa ni pamoja na kipindupindu, malaria, ugonjwa wa surua, yellow fever, polio na kimeta, ambayo yote yanahusisha moja kwa moja na hali mbaya ya hew ana hii inaathiri pakubwa mifumo ya Uchumi katika pembe ya afrika.
IGAD imesema kuwa Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan na Uganda zinashughulikia milipuko ya kipindupindu, iliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni. Nchini Ethiopia, visa 14,632 na vifo 114 viliripotiwa kutoka maeneo 90 katika mikoa 11 kati ya tarehe 1 mwezi Januari hadi tarehe 28 mwezi Aprili.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































